Sunday, September 22, 2013

AMRI YA RAIS JK KUHUSU WAHAMIAJI HARAMU !

Wananchi washirikishwe katika kuwafichua wahamiaji haramu na kuwa ripoti katika vyombo vya dola !
Katika kutekeleza agizo la Rais Jakaya Kikwete kuwataka wahamiaji wote haramu
waondoke nchini,kuna haja kubwa ya wananchi kushirikiana vyombo vya dola katika kuwafichua wahamiaji hao haramu ,kwa kuwashirikisha wananchi kazi ya kusafisha maovu na uvunjwaji wa amani unasababishwa na wahamiaji hao itafanikiwa kwa kasi kubwa.
Kama vyombo vya dola vitawashirikisha wananchi na viongozi wa mashina katika serikali za mitaa zoezi hili litafanikiwa kwa haraka sana.

Mkuu wa nchi ambaye ndiye amri jeshi mkuu mwenye majukumu makubwa nchini
Rais Dkt.JK kuanzia mwezi Julai 2013 alitoa agizo la siku 14 kwa wahamiaji wote haramu kuondoka nchini au kujisalimisha kwa vyombo vya dola,lakini hadi sasa
wahamiaji walioondoka ni wachache na wengi wao bado wanajifaragua mitaani
huku vyombo vya dola vikiwatazama.
Kwanini ? agizo hili la Rais JK lisiliwashirikishe wananchi,madiwani,wakuu wa mikoa na wilaya,wenyeviti wa serikali za mitaa .
kazi ifanyike kwa haraka.
Mungu Ibariki Tanzania
Mungu mbariki Rais JK