Sunday, April 13, 2014

Umoja wa waTanzania Ujerumani (UTU) kufanya mkutato mkuu wa Uchaguzi 26.April 2014 Berlin






Berlin,Ujerumani,
Umoja wa Watanzania Ujerumani (UTU) unatarajia kufanya mkutano wake mkuu  wa uchaguzi siku ya kilele cha sherehe za muunganno wa Tanzania mjini Berlin, Ujerumani. siku ya tarehe 26.April.2014 kuanzia saa 7 mchana katika ukumbi wa Deutsche Bank, Unter den Linden 13-15, 10117 Berlin, Ujerumani.
Watanzania wote wanaoishi Ujerumani wanaombwa kuhudhuria kwa wingi katika mkutano huu muhimu wa chombo chao UTU ambao kinawaunganisha watanzania wote waishio ujerumani bila kujali itikadi zao za kidini, jinsia, wala kabila.
Umoja wa watanzania ujerumani unafuraha kubwa ya kuwafungilia milango wale wote ambao wanataka kujiunga na umoja huo. Pia milango ipo wazi kwa wadau na wale wote wanaohitaji ushauri juu ya kuwekeza au kuchangia maendeleo ya jamii nyumbani Tanzania.
Pia pata kuwepo na vyakula vya kitanzania

KUFIKA KWENU KATIKA MKUTANO HUU NDIO MAFANIKIO YA WATANZANIA WOTE

UMOJA NI NGUVU , UTENGANO NI UDHAIFU

UMOJA WA KITAIFA NDIO MSINGI IMARA KWA WATANZANIA
MUNGU IBARIKI TANZANIA

NGOMA AFRICA BAND YA UJERUMANI YATOA RAMBI RAMBI KUFUATIA KIFO CHA MWANA MUZIKI MKONGWE MUHIDIN GURUMO (RIP)

Tumepokea kwa udhuni na majonzi makubwa taarifa ya kifo cha mkongwe wa muziki wa dansi nchini Tanzania na Africa ya mashariki marehemu mzee Muhidin Maalimu Gurumo Kilichotokea leo 13.04.2014 huko nyumbani Tanzania.Pamoja na kuwa mbali na nyumbani bendi ya muziki wa dansi Ngoma Africa Band yenye makao yake nchini Ujerumani  inaungana na watanzania wote popote pale katika kuomboleza msiba huu.
Tunatoa pole zetu kwa bendi ya Msondo Ngoma pamoja na familia ya marehemu,mwenyezi mungu
amlaze mahala pema peponi marehemu Mzee Muhidin Maalim
Gurumo (RIP)
Amin