Monday, October 29, 2012
Saturday, October 27, 2012
Watanzania wa Ujerumani Kukutana na wafadhili zaidi ya 150 ! huko Mainashaff,Ujerumani
UNION OF TANZANIANS IN GERMANY (UTU)
KUKUTANA NA WAFADHILI NA WAHISANI ZAIDI YA 150 !!!!
KUKUTANA NA WAFADHILI NA WAHISANI ZAIDI YA 150 !!!!
WORLD MISSION SUNDAY 28.OCT. 2012
Umoja wa Watanzania Ujerumani (UTU)
Unapenda kuwakaribisha Watanzania
wote wanaoishi ujerumani, Katika Hafla ya WORLD MISSION SUNDAY. itakayofanyika Katika ukumbi Uliopo Hauptstr.
30, D-63814 Mainaschaff Jirani sana na Mji wa Aschaffenburg Siku ya
Jumapili Tarehe 28.10.2012,
Kuanzia saa 04:00 za Asubuhi. Ambapo Wasamaria wema na Wafadhili
wapatao zaidi ya 150 kutoka sehemu mbali mbali za ujerumani watakutana
na umoja wa Watanzania Ujerumani (UTU) Juu ya kuitakia mema Tanzania na
kuanzisha Harambee ya kuchangia maendeleo ya miradi mbali mbali
itakayosimamiwa na Umoja wa watanzania Ujerumani (UTU). Katika Hafla
hiyo Kuanzia saa 9 mchana watayarishaji wa Hafla hiyo ''World Mission Sunday''
itatoa nafasi kwa Umoja wa Watanzania Ujermani (UTU) Kuitambulisha
Tanzania Kwa wahisani hao , na kuelezea ni mradi gani unahitaji
ufadhili kupitia Umoja huu. Mmoja wa wageni rasmi walio alikuwa ni
Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Mhe. Ahmada Ngemera, Dr. Lippert na mkewe Kutoka Scheinfurt' Dr.
Lippert ni mtaalamu ambaye aliwahi kufanya kazi Tanzania. Hafla hii
inategemewa kuisha saa 12:00 za jioni, baada ya hapo watanzania watapata
muda wao wa kufanya mazungumzo na Mhe: Balozi wa Tanzania
Nchini ujerumani Bw. Ahmada Ngemera.
Umoja wa Watanzania Ujerumani UTU Umeramba Bingo kwa kupewa nafasi hii ya pekee Na WORLD MISSION SUNDAY Kuiwakilisha Jamii ya watanzania na kuwashawishi Wafadhili na wahisani nchini ujerumani ili waweze kuchangia Miradi mbali mbali ya Huduma za jamii nchni Tanzania ikiwemo sekta ya Elimu na Afya.
Tunawaomba Watanzania Wote na marafiki wa Tanzania wanaoishi Ujerumani na jirani mwa ujerumani, kuhudhuria kwa wingi katika Hafla hii muhimu kwa jamii ya watanzani kama wasemavyo wahenga ''CHEREKO CHEREKO NA MWENYE MWANA'' Kwa maelezo zaidi wasiliana na kamati.utu@googlemail.com au unaweza kuwasiliana na Mwenyekiti Wa UTU moja kwa moja kupitia simu ya mkononi. 0173-4298997
Umoja wa Watanzania Ujerumani UTU Umeramba Bingo kwa kupewa nafasi hii ya pekee Na WORLD MISSION SUNDAY Kuiwakilisha Jamii ya watanzania na kuwashawishi Wafadhili na wahisani nchini ujerumani ili waweze kuchangia Miradi mbali mbali ya Huduma za jamii nchni Tanzania ikiwemo sekta ya Elimu na Afya.
Tunawaomba Watanzania Wote na marafiki wa Tanzania wanaoishi Ujerumani na jirani mwa ujerumani, kuhudhuria kwa wingi katika Hafla hii muhimu kwa jamii ya watanzani kama wasemavyo wahenga ''CHEREKO CHEREKO NA MWENYE MWANA'' Kwa maelezo zaidi wasiliana na kamati.utu@googlemail.com au unaweza kuwasiliana na Mwenyekiti Wa UTU moja kwa moja kupitia simu ya mkononi. 0173-4298997
Karibuni sana ! Umoja Ni Nguvu
Tuesday, October 2, 2012
Monday, October 1, 2012
Dantiz Ft GQ - Near By ( Final-Official).
listening to Dantiz Ft GQ - Near By ( Final-Official)... click here for download or listening
Pata kumsikiliza dantiz walii na kitu chake kimya kabisa near by u kutoka Racers ngoma imeenda mbele sana
Pata kumsikiliza dantiz walii na kitu chake kimya kabisa near by u kutoka Racers ngoma imeenda mbele sana
Umoja wa watanzania Ujerumani wapata Uongozi Mpya
Naibu Balozi Mh.Ali Siwa (mwenye suti nyeusi) akiwa na viongozi wa UTU. |
watanzaia Ujerumani wakiwa na furaha ya umoja wao |
Kamanda Ras makunja katikati,akipigwa pini na Sudu Mnete wa Radio DW (mwenye nyeusi na nyeupe) Mdau Elezius naye pembeni |
Meza kuu katika mkutano wa Umoja wa watanzania Ujerumani. |
Mhe.Bw.Ali Siwa (mwenye suti nyeusi) akiwa na viongozi wa UTU |
Mwanadiplomasia Naibu balozi Bw.Ali Siwa (katikati)akiongea na watanzania. |
Watanzania Ujerumani wakiduarika |
huyu bint mdogo naye alikuapo |
Sudu Mnete wa Radio DW (mwenye nyeusi na nyeupe)akiwa na viongozi wa UTU |
Mkutano
mkuu wa watanzania waishio ujerumani uliofanyika siku ya jumaamosi
tarehe 29. 09 2012 Mjini Frankfurt katika kitongoji cha Raunheim.
ulifanikiwa kutimiza malengo yake na maazimio yake Moja wapo ilikuwa ni
kufanya uchaguzi wa uongozi wa umoja huo, kabla ya kufanyika uchaguzi
huo na mjadala wa maazimio ya umoja huo, Mgeni rasmi katika mkutano huo
mwana diplomasia naibu balozi wa Tanzania
nchini ujerumani mheshimiwa Bw. Ali Siwa alitoa nasaha zake na salamu
kutoka Ubalozi wa Tanzania Nchini ujerumani kwa watanzania waliohudhuria
katika mkutano huo, kwanza aliwapongeza watanzania kwa kufanikiwa
kuunda umoja huo wa watanzania waishio
ujerumani ambao ndio mwamvuli mkuu wa mshikamano wa watanzania wote
nchini ujeruman, isitoshe Bw. Ali Siwa aliwaambia watanzania kwamba
ofisi yake ipo wazi wakati wowote iwapo umoja huo utahitaji ushauri
wowote utakaoleta maendeleo ya umoja huo na watanzania kwa ujumla,
aliwaasa watanzania kuwa mshikamano wao na umoja wao ndio utakaokuwa
ufunguo na sauti ya maendeleo yao na vizazi vwao ugenini na nyumbani
pia. baada ya nasaha hizo wananchama wa umoja wa watanzania walichagua
viongozi wao kama ifuatavyo:-
Mwenyekiti:
Mfundo Peter Mfundo, Makamo: M/Mwenyekiti. George Mtalemwa. Katibu: Bi
Tulalumba Mloge. Muweka hazina: Bi Mwamvua Dugala Merkel.
Umoja
huo wa Watanzania Ujerumani (UTU) ndio chombo pekee kilichopata usajili
kwenye serikali ya ujerumani, na kutambuliwa kisheria, ambacho
kinawaunganisha watanzania wote wanaoishi ujerumani, na ndio Daraja
linalowaunganisha watanzania waliopo Nyumbani na kwengineko ughaibuni.
Kwa watanzania wanaopenda kujiunga na umoja wa watanzania ujerumani
(UTU) milango ipo wazi, wasiliana na kamati.utu@googlemail.com
Subscribe to:
Posts (Atom)