Wananchi washirikishwe katika kuwafichua wahamiaji haramu na kuwa ripoti katika vyombo vya dola !
Katika kutekeleza agizo la Rais Jakaya Kikwete kuwataka wahamiaji wote haramu
waondoke nchini,kuna haja kubwa ya wananchi kushirikiana vyombo vya
dola katika kuwafichua wahamiaji hao haramu ,kwa kuwashirikisha
wananchi kazi ya kusafisha maovu na uvunjwaji wa amani unasababishwa na
wahamiaji hao itafanikiwa kwa kasi kubwa.
Kama vyombo vya dola vitawashirikisha wananchi na viongozi wa
mashina katika serikali za mitaa zoezi hili litafanikiwa kwa haraka
sana.
Mkuu wa nchi ambaye ndiye amri jeshi mkuu mwenye majukumu makubwa nchini
Rais Dkt.JK kuanzia mwezi Julai 2013 alitoa agizo la siku 14 kwa
wahamiaji wote haramu kuondoka nchini au kujisalimisha kwa vyombo vya
dola,lakini hadi sasa
wahamiaji walioondoka ni wachache na wengi wao bado wanajifaragua mitaani
huku vyombo vya dola vikiwatazama.
Kwanini ? agizo hili la Rais JK lisiliwashirikishe wananchi,madiwani,wakuu wa mikoa na wilaya,wenyeviti wa serikali za mitaa .
kazi ifanyike kwa haraka.
Mungu Ibariki Tanzania