Wednesday, December 19, 2012
Saturday, December 1, 2012
Monday, October 29, 2012
Saturday, October 27, 2012
Watanzania wa Ujerumani Kukutana na wafadhili zaidi ya 150 ! huko Mainashaff,Ujerumani
UNION OF TANZANIANS IN GERMANY (UTU)
KUKUTANA NA WAFADHILI NA WAHISANI ZAIDI YA 150 !!!!
KUKUTANA NA WAFADHILI NA WAHISANI ZAIDI YA 150 !!!!
WORLD MISSION SUNDAY 28.OCT. 2012
Umoja wa Watanzania Ujerumani (UTU)
Unapenda kuwakaribisha Watanzania
wote wanaoishi ujerumani, Katika Hafla ya WORLD MISSION SUNDAY. itakayofanyika Katika ukumbi Uliopo Hauptstr.
30, D-63814 Mainaschaff Jirani sana na Mji wa Aschaffenburg Siku ya
Jumapili Tarehe 28.10.2012,
Kuanzia saa 04:00 za Asubuhi. Ambapo Wasamaria wema na Wafadhili
wapatao zaidi ya 150 kutoka sehemu mbali mbali za ujerumani watakutana
na umoja wa Watanzania Ujerumani (UTU) Juu ya kuitakia mema Tanzania na
kuanzisha Harambee ya kuchangia maendeleo ya miradi mbali mbali
itakayosimamiwa na Umoja wa watanzania Ujerumani (UTU). Katika Hafla
hiyo Kuanzia saa 9 mchana watayarishaji wa Hafla hiyo ''World Mission Sunday''
itatoa nafasi kwa Umoja wa Watanzania Ujermani (UTU) Kuitambulisha
Tanzania Kwa wahisani hao , na kuelezea ni mradi gani unahitaji
ufadhili kupitia Umoja huu. Mmoja wa wageni rasmi walio alikuwa ni
Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Mhe. Ahmada Ngemera, Dr. Lippert na mkewe Kutoka Scheinfurt' Dr.
Lippert ni mtaalamu ambaye aliwahi kufanya kazi Tanzania. Hafla hii
inategemewa kuisha saa 12:00 za jioni, baada ya hapo watanzania watapata
muda wao wa kufanya mazungumzo na Mhe: Balozi wa Tanzania
Nchini ujerumani Bw. Ahmada Ngemera.
Umoja wa Watanzania Ujerumani UTU Umeramba Bingo kwa kupewa nafasi hii ya pekee Na WORLD MISSION SUNDAY Kuiwakilisha Jamii ya watanzania na kuwashawishi Wafadhili na wahisani nchini ujerumani ili waweze kuchangia Miradi mbali mbali ya Huduma za jamii nchni Tanzania ikiwemo sekta ya Elimu na Afya.
Tunawaomba Watanzania Wote na marafiki wa Tanzania wanaoishi Ujerumani na jirani mwa ujerumani, kuhudhuria kwa wingi katika Hafla hii muhimu kwa jamii ya watanzani kama wasemavyo wahenga ''CHEREKO CHEREKO NA MWENYE MWANA'' Kwa maelezo zaidi wasiliana na kamati.utu@googlemail.com au unaweza kuwasiliana na Mwenyekiti Wa UTU moja kwa moja kupitia simu ya mkononi. 0173-4298997
Umoja wa Watanzania Ujerumani UTU Umeramba Bingo kwa kupewa nafasi hii ya pekee Na WORLD MISSION SUNDAY Kuiwakilisha Jamii ya watanzania na kuwashawishi Wafadhili na wahisani nchini ujerumani ili waweze kuchangia Miradi mbali mbali ya Huduma za jamii nchni Tanzania ikiwemo sekta ya Elimu na Afya.
Tunawaomba Watanzania Wote na marafiki wa Tanzania wanaoishi Ujerumani na jirani mwa ujerumani, kuhudhuria kwa wingi katika Hafla hii muhimu kwa jamii ya watanzani kama wasemavyo wahenga ''CHEREKO CHEREKO NA MWENYE MWANA'' Kwa maelezo zaidi wasiliana na kamati.utu@googlemail.com au unaweza kuwasiliana na Mwenyekiti Wa UTU moja kwa moja kupitia simu ya mkononi. 0173-4298997
Karibuni sana ! Umoja Ni Nguvu
Tuesday, October 2, 2012
Monday, October 1, 2012
Dantiz Ft GQ - Near By ( Final-Official).
listening to Dantiz Ft GQ - Near By ( Final-Official)... click here for download or listening
Pata kumsikiliza dantiz walii na kitu chake kimya kabisa near by u kutoka Racers ngoma imeenda mbele sana
Pata kumsikiliza dantiz walii na kitu chake kimya kabisa near by u kutoka Racers ngoma imeenda mbele sana
Umoja wa watanzania Ujerumani wapata Uongozi Mpya
Naibu Balozi Mh.Ali Siwa (mwenye suti nyeusi) akiwa na viongozi wa UTU. |
watanzaia Ujerumani wakiwa na furaha ya umoja wao |
Kamanda Ras makunja katikati,akipigwa pini na Sudu Mnete wa Radio DW (mwenye nyeusi na nyeupe) Mdau Elezius naye pembeni |
Meza kuu katika mkutano wa Umoja wa watanzania Ujerumani. |
Mhe.Bw.Ali Siwa (mwenye suti nyeusi) akiwa na viongozi wa UTU |
Mwanadiplomasia Naibu balozi Bw.Ali Siwa (katikati)akiongea na watanzania. |
Watanzania Ujerumani wakiduarika |
huyu bint mdogo naye alikuapo |
Sudu Mnete wa Radio DW (mwenye nyeusi na nyeupe)akiwa na viongozi wa UTU |
Mkutano
mkuu wa watanzania waishio ujerumani uliofanyika siku ya jumaamosi
tarehe 29. 09 2012 Mjini Frankfurt katika kitongoji cha Raunheim.
ulifanikiwa kutimiza malengo yake na maazimio yake Moja wapo ilikuwa ni
kufanya uchaguzi wa uongozi wa umoja huo, kabla ya kufanyika uchaguzi
huo na mjadala wa maazimio ya umoja huo, Mgeni rasmi katika mkutano huo
mwana diplomasia naibu balozi wa Tanzania
nchini ujerumani mheshimiwa Bw. Ali Siwa alitoa nasaha zake na salamu
kutoka Ubalozi wa Tanzania Nchini ujerumani kwa watanzania waliohudhuria
katika mkutano huo, kwanza aliwapongeza watanzania kwa kufanikiwa
kuunda umoja huo wa watanzania waishio
ujerumani ambao ndio mwamvuli mkuu wa mshikamano wa watanzania wote
nchini ujeruman, isitoshe Bw. Ali Siwa aliwaambia watanzania kwamba
ofisi yake ipo wazi wakati wowote iwapo umoja huo utahitaji ushauri
wowote utakaoleta maendeleo ya umoja huo na watanzania kwa ujumla,
aliwaasa watanzania kuwa mshikamano wao na umoja wao ndio utakaokuwa
ufunguo na sauti ya maendeleo yao na vizazi vwao ugenini na nyumbani
pia. baada ya nasaha hizo wananchama wa umoja wa watanzania walichagua
viongozi wao kama ifuatavyo:-
Mwenyekiti:
Mfundo Peter Mfundo, Makamo: M/Mwenyekiti. George Mtalemwa. Katibu: Bi
Tulalumba Mloge. Muweka hazina: Bi Mwamvua Dugala Merkel.
Umoja
huo wa Watanzania Ujerumani (UTU) ndio chombo pekee kilichopata usajili
kwenye serikali ya ujerumani, na kutambuliwa kisheria, ambacho
kinawaunganisha watanzania wote wanaoishi ujerumani, na ndio Daraja
linalowaunganisha watanzania waliopo Nyumbani na kwengineko ughaibuni.
Kwa watanzania wanaopenda kujiunga na umoja wa watanzania ujerumani
(UTU) milango ipo wazi, wasiliana na kamati.utu@googlemail.com
Tuesday, September 4, 2012
Michael Clarke Duncan has passed away at the age of 54
Oscar-nominated actor Michael Clarke Duncan has passed away at the age of 54, according to his fiancée Omarosa Stallworth and news reports on the wire. Duncan suffered a heart attack on July 13 and according to his publicist, he never fully recovered from it.
After a number of years doing television and small movie roles, Michael Clarke Duncan first got the attention of moviegoers when he was cast in the role of inmate John Coffey in Frank Darabont's 2000 prison drama The Green Mile, giving a performance opposite Tom Hanks that would earn him an Oscar nomination at the age of 43.
From there, he was paired with Bruce Willis and Matt Perry in the 1999 comedy The Whole Nine Yards, which spawned the sequel The Whole Ten Yards, but the 6' 5" Clarke Duncan found most of his success appearing in genre films. From Tim Burton's remake of Planet of the Apes to Frank Miller and Robert Rodriguez's Sin CIty, from playing the Kingpin in Daredevil to Michael Bay's Armageddon and The Island andStreet Fighter: The Legend of Chu-Li, Clarke Duncan's impressive size always made him a presence on the screen.
On top of that, the actor had an unmistakable voice that could be heard in numerous animated shows and films, including "Teen Titans," Kung Fu Panda and providing the voice of Kilowo
Friday, August 24, 2012
Ben Pol-Pete mp3.
listening to Ben Pol-Pete mp3.mp3. click here
Its ur boy ben pol came wiz new song pete a good R&B song
Its ur boy ben pol came wiz new song pete a good R&B song
Deddy-Bashment tym
listening to Deddy-Bashment tym.mp3.click here
Now amekuja na single yake mwenyewe baada ya kupiga kazi na kundi lake la uknown na kutoa kibao cha sorry bila kusahau ile track pamoja we can ya dj choka sasa anakuja na kitu bashment it's ur boy Deddy goma lipo katikas radha ya dancehall limefanywa sinza kwenye studio ya feel good record
Now amekuja na single yake mwenyewe baada ya kupiga kazi na kundi lake la uknown na kutoa kibao cha sorry bila kusahau ile track pamoja we can ya dj choka sasa anakuja na kitu bashment it's ur boy Deddy goma lipo katikas radha ya dancehall limefanywa sinza kwenye studio ya feel good record
UNKNOWNSORRYProducedByPANCHOMixedMastere
listening to UNKNOWNSORRYProducedByPANCHOMixedMastere..click here.
Unataka swagger za ukweli kabisa basi click link juu yako upate kuwasikiliza vijana hatari kabisa unknown na tack yao ya Sorry, kundi hilo ambalo lina vijana wa nne tu ambao no king of salasala King Zilla,Deddy,Gosby na Pancho latino
Thursday, August 23, 2012
DK MWAKYEMBE AMSIMAMISHA MKURUGENZI MKUU, WENGINE WATANO,AANIKA UFISADI, RUSHWA, WIZI WA MAFUTA
WAZIRI wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe amemsimamisha kazi
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Ephraim Mgawe, wasaidizi
wake wawili na Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Cassian Ng'amilo kupisha
uchunguzi wa wizi wa vitu mbalimbali yakiwamo makontena 40 ya vitenge, katika
Bandari ya Dar es Salaam.
Dk Mwakyembe alitangaza uamuzi wake huo jana jijini Dar es Salaam, akiendeleza kile alichokifanya Juni 5 mwaka huu alipomtimua kazi aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), Paul Chizi.
Hata hivyo, waziri huyo hakutaja majina ya vigogo waliosimamishwa na badala yake alitaja nafasi walizokuwa wakizishikilia ambazo ni pamoja na Meneja wa Kituo cha Mafuta ya Ndege Kurasini (Kurasini Oil Jet - KOJ), Meneja wa Kituo cha Mafuta JET na mhandisi wa mafuta wa kituo hicho, baada ya kubainika kuwapo kwa wizi wa mafuta.
Kutokana na uamuzi huo, Dk Mwakyembe amemteua Mkurugenzi wa Usalama na Mazingira katika Wizara ya Ujenzi, Injinia Madeni Kipande kukaimu nafasi ya Mgawe.
Gazeti hili lilimtafuta Mgawe kwa simu kuzungumzia uamuzi huo, lakini simu yake ya mkononi ilikuwa ikiita muda wote bila majibu na wakati mwingine kukatwa.
Uamuzi huo umekuja baada ya kuwapo kwa taarifa za kupotea kwa makontena takriban 40 ya vitenge na vitu mbalimbali, yaliyokuwa yakipelekwa nchi jirani.
Dk Mwakyembe alisema ameunda kamati ya watu saba ambao hakuwataja majina ili kuchunguza wizi huo na kwamba amewapa wiki mbili tu, wawe wamekamilisha kazi hiyo.
“Nimeunda kamati ya kuchunguza suala hili, nimewapa hadidu za rejea zenye maswali 50..., majina ya waliopo katika kamati hii siyatangazi kwa sasa kwa sababu zangu binafsi,” alisema Dk Mwakyembe.
Alisema amechukua uamuzi huo baada ya kukutana na Bodi ya Wakurugenzi ya TPA juzi na kwamba hawezi kuvumilia kuona nchi inakosa mapato kwa sababu ya wizi uliokithiri.
Alisema kwa muda mrefu katika bandari hiyo ya Dar es Salaam, kumekuwa na malalamiko ya wizi wa vitu mbalimbali, ikiwa ni pamoja na ule wa vifaa vya magari, mafuta na kukithiri rushwa.
Alifafanua kwamba wizi huo umesababisha Bandari ya Dar es Salaam kukimbiwa na wateja ambao hivi sasa wanatumia bandari za Kenya, Msumbiji na Afrika Kusini.
“Makontena yanaibwa kama njugu, hivi sasa watu wa Rwanda, Uganda DRC hawaitumii tena Bandari ya Dar es Salaam, wanaona bora waingie hasara na wameanza kupitisha mizigo yao katika Bandari ya Mombasa Kenya, Beira nchini Msumbiji na Durban Afrika Kusini,” alisema Dk Mwakyembe.
Dk Mwakyembe alisema kuwa hivi karibuni mfanyabiashara mmoja mwanamke alitishia kuhamia nyumbani kwake, baada ya kuibiwa kontena zima la vitenge vilivyokuwa na thamani ya dola 180,000 za Marekani.
“Ni mambo ya ajabu sana hatuwezi kuwa na maendeleo kwa masuala ya ‘kisanii’ kama haya, nimeamua hivi kutokana na mamlaka niliyonayo na uamuzi nitakaouchukua najua wenzangu watanielewa,” alisema.
Wakati akieleza majukumu ya Mamlaka hiyo alisema, “Nimewataka TPA watambue majukumu yao jinsi yalivyo nyeti, nimewaeleza wazi kuwa imani ya wananchi imepungua sana kwa mamlaka hiyo.
“Kama waziri mwenye dhamana sitakuwa tayari kuona jambo hili linaendelea, hili suala haliwezi kuachwa likaendelea ni lazima uchunguzi ufanyike.”
Dk Mwakyembe alisema kuwa ameiagiza bodi ya wakurugenzi, kitengo cha sheria TPA kiuchambue upya mkataba wa Kampuni ya Kupakia na Kupakua Makontena katika Bandari ya Dar es Salaam (Ticts) na kumpatia taarifa Jumatano ijayo.
“Kontena likiwa na vitenge hata ukiweka askari 40 linaondoka, tumepoteza wateja wengi na watu wanaona bora kukimbilia bandari nyingine, nimewaagiza wauchambue upya mkataba huu,” alisema Dk Mwakyembe.
Agizo
Alisema ili kukomesha rushwa ameitaka Bodi ya Wakurugenzi TPA, kuanzia Septemba mosi mwaka huu kuacha kutumia utaratibu wa kulipa fedha dirishani, badala yake fedha zote zilipwe kupitia benki.
“Mtindo wa malipo ya fedha dirishani ndiyo unachochea wizi unaofanywa na mtandao wa kisanii pale TPA. Nimeagiza malipo yote yafanyike kupitia benki au kwa njia zozote za teknohama kuanzia Septemba mosi,” alisema Dk Mwakyembe na kuongeza:
“Kama malipo haya yakiendelea mwezi ujao watakaolipa waandike tu wenyewe barua za kuacha kazi, kampuni ndogondogo nchini zinalipa fedha kupitia benki, kwa nini TPA washindwe?”
Aliongeza kuwa ameiagiza bodi hiyo kuangalia upya mfumo mzima wa uongozi wa TPA na bandari kwa kuwa kuna viongozi wana mamlaka makubwa wakati vyeo vyao ni vidogo.
“Meneja wa bandari ana mamlaka makubwa kiasi kwamba utendaji kazi ndani ya bandari unasuasua wakati wapo viongozi wa juu yake,” alisema Dk Mwakyembe.
Wizi wa mafuta
Akizungumzia wizi wa mafuta, Dk Mwakyembe alisema katika kituo cha KOJ kuna wizi mkubwa wa mafuta ambapo wahusika wakibanwa hutoa kisingizio kuwa mafuta yanayochukuliwa ni machafu.
“Mafuta yale siyo machafu, hiyo imekuwa ndiyo biashara yao kila mwaka, ndiyo maana tenda ya mafuta machafu inagombewa sana, tumefuatilia na kugundua kuwa yanapelekwa katika vituo mbalimbali vya mafuta nchini” alisema Mwakyembe na kuongeza:
“Niliwahi kwenda katika eneo lile saa 12 asubuhi na kukuta malori yanajaza mafuta. Niliuliza lori lina uwezo wa kupakia lita ngapi, kuanzia meneja mpaka watu wa chini kabisa walishindwa kunijibu.”
Alisema kutokana na kitendo hicho, amechukua sampuli ya mafuta hayo na kuyapeleka Mombasa, Kenya kuyapima ili kugundua yana kiwango cha mafuta masafi kwa asilimia ngapi.
Alisema kuwa malori hayo yana uwezo wa kupakia lita 26,000 za mafuta lakini wahusika wanadai kuwa yanaweza kupakia lita 9,000 tu.
“Mafuta haya huibwa wakati yakitolewa katika meli na kupelekwa katika magari, karibu asilimia mbili nzima ya mafuta huibwa, kiwango ambacho ni kikubwa sana,” alisema.
Alisema kutokana na hali hiyo ameagiza kurejeshwa kwa kifaa cha kupimia wingi wa mafuta katika malori ya mafuta, ndani ya mwezi mmoja kuanzia jana.
Aanika ufisadi
Alisema kampuni ya Singirimo iliyopewa zabuni ya kusafirisha mafuta machafu, mkataba wake ulishaisha siku nyingi, lakini bado inaendelea na kazi hiyo na kwamba mwaka 2008, Ikulu iliwahi kueleza kuwa kampuni hiyo ni kinara kwa kusafirisha mafuta masafi na kudai machafu.
“Kampuni hii kila mwaka inashinda tenda ya kusafirisha mafuta tu, hivi sasa inachunguzwa na Ewura na Takukuru, nimeagiza mamlaka husika kwamba kampuni hii isijihusishe tena na usafirishaji wa mafuta ili kupisha uchunguzi,” alisema Dk Mwakyembe na kuongeza:
“Kampuni iliyokuwa namba mbili katika utoaji wa tenda ndiyo ipewe jukumu hilo na kama isipopewa ndiyo nitajua kuna kitu kinaendelea.”
Alisema kuwa mwaka 2008 Ikulu ilisema kuwa kampuni ya Singirimo ni ya wafanyakazi na vigogo wa TPA na inasafirisha mafuta masafi na kudai kuwa ni machafu.
Dk Mwakyembe alitangaza uamuzi wake huo jana jijini Dar es Salaam, akiendeleza kile alichokifanya Juni 5 mwaka huu alipomtimua kazi aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), Paul Chizi.
Hata hivyo, waziri huyo hakutaja majina ya vigogo waliosimamishwa na badala yake alitaja nafasi walizokuwa wakizishikilia ambazo ni pamoja na Meneja wa Kituo cha Mafuta ya Ndege Kurasini (Kurasini Oil Jet - KOJ), Meneja wa Kituo cha Mafuta JET na mhandisi wa mafuta wa kituo hicho, baada ya kubainika kuwapo kwa wizi wa mafuta.
Kutokana na uamuzi huo, Dk Mwakyembe amemteua Mkurugenzi wa Usalama na Mazingira katika Wizara ya Ujenzi, Injinia Madeni Kipande kukaimu nafasi ya Mgawe.
Gazeti hili lilimtafuta Mgawe kwa simu kuzungumzia uamuzi huo, lakini simu yake ya mkononi ilikuwa ikiita muda wote bila majibu na wakati mwingine kukatwa.
Uamuzi huo umekuja baada ya kuwapo kwa taarifa za kupotea kwa makontena takriban 40 ya vitenge na vitu mbalimbali, yaliyokuwa yakipelekwa nchi jirani.
Dk Mwakyembe alisema ameunda kamati ya watu saba ambao hakuwataja majina ili kuchunguza wizi huo na kwamba amewapa wiki mbili tu, wawe wamekamilisha kazi hiyo.
“Nimeunda kamati ya kuchunguza suala hili, nimewapa hadidu za rejea zenye maswali 50..., majina ya waliopo katika kamati hii siyatangazi kwa sasa kwa sababu zangu binafsi,” alisema Dk Mwakyembe.
Alisema amechukua uamuzi huo baada ya kukutana na Bodi ya Wakurugenzi ya TPA juzi na kwamba hawezi kuvumilia kuona nchi inakosa mapato kwa sababu ya wizi uliokithiri.
Alisema kwa muda mrefu katika bandari hiyo ya Dar es Salaam, kumekuwa na malalamiko ya wizi wa vitu mbalimbali, ikiwa ni pamoja na ule wa vifaa vya magari, mafuta na kukithiri rushwa.
Alifafanua kwamba wizi huo umesababisha Bandari ya Dar es Salaam kukimbiwa na wateja ambao hivi sasa wanatumia bandari za Kenya, Msumbiji na Afrika Kusini.
“Makontena yanaibwa kama njugu, hivi sasa watu wa Rwanda, Uganda DRC hawaitumii tena Bandari ya Dar es Salaam, wanaona bora waingie hasara na wameanza kupitisha mizigo yao katika Bandari ya Mombasa Kenya, Beira nchini Msumbiji na Durban Afrika Kusini,” alisema Dk Mwakyembe.
Dk Mwakyembe alisema kuwa hivi karibuni mfanyabiashara mmoja mwanamke alitishia kuhamia nyumbani kwake, baada ya kuibiwa kontena zima la vitenge vilivyokuwa na thamani ya dola 180,000 za Marekani.
“Ni mambo ya ajabu sana hatuwezi kuwa na maendeleo kwa masuala ya ‘kisanii’ kama haya, nimeamua hivi kutokana na mamlaka niliyonayo na uamuzi nitakaouchukua najua wenzangu watanielewa,” alisema.
Wakati akieleza majukumu ya Mamlaka hiyo alisema, “Nimewataka TPA watambue majukumu yao jinsi yalivyo nyeti, nimewaeleza wazi kuwa imani ya wananchi imepungua sana kwa mamlaka hiyo.
“Kama waziri mwenye dhamana sitakuwa tayari kuona jambo hili linaendelea, hili suala haliwezi kuachwa likaendelea ni lazima uchunguzi ufanyike.”
Dk Mwakyembe alisema kuwa ameiagiza bodi ya wakurugenzi, kitengo cha sheria TPA kiuchambue upya mkataba wa Kampuni ya Kupakia na Kupakua Makontena katika Bandari ya Dar es Salaam (Ticts) na kumpatia taarifa Jumatano ijayo.
“Kontena likiwa na vitenge hata ukiweka askari 40 linaondoka, tumepoteza wateja wengi na watu wanaona bora kukimbilia bandari nyingine, nimewaagiza wauchambue upya mkataba huu,” alisema Dk Mwakyembe.
Agizo
Alisema ili kukomesha rushwa ameitaka Bodi ya Wakurugenzi TPA, kuanzia Septemba mosi mwaka huu kuacha kutumia utaratibu wa kulipa fedha dirishani, badala yake fedha zote zilipwe kupitia benki.
“Mtindo wa malipo ya fedha dirishani ndiyo unachochea wizi unaofanywa na mtandao wa kisanii pale TPA. Nimeagiza malipo yote yafanyike kupitia benki au kwa njia zozote za teknohama kuanzia Septemba mosi,” alisema Dk Mwakyembe na kuongeza:
“Kama malipo haya yakiendelea mwezi ujao watakaolipa waandike tu wenyewe barua za kuacha kazi, kampuni ndogondogo nchini zinalipa fedha kupitia benki, kwa nini TPA washindwe?”
Aliongeza kuwa ameiagiza bodi hiyo kuangalia upya mfumo mzima wa uongozi wa TPA na bandari kwa kuwa kuna viongozi wana mamlaka makubwa wakati vyeo vyao ni vidogo.
“Meneja wa bandari ana mamlaka makubwa kiasi kwamba utendaji kazi ndani ya bandari unasuasua wakati wapo viongozi wa juu yake,” alisema Dk Mwakyembe.
Wizi wa mafuta
Akizungumzia wizi wa mafuta, Dk Mwakyembe alisema katika kituo cha KOJ kuna wizi mkubwa wa mafuta ambapo wahusika wakibanwa hutoa kisingizio kuwa mafuta yanayochukuliwa ni machafu.
“Mafuta yale siyo machafu, hiyo imekuwa ndiyo biashara yao kila mwaka, ndiyo maana tenda ya mafuta machafu inagombewa sana, tumefuatilia na kugundua kuwa yanapelekwa katika vituo mbalimbali vya mafuta nchini” alisema Mwakyembe na kuongeza:
“Niliwahi kwenda katika eneo lile saa 12 asubuhi na kukuta malori yanajaza mafuta. Niliuliza lori lina uwezo wa kupakia lita ngapi, kuanzia meneja mpaka watu wa chini kabisa walishindwa kunijibu.”
Alisema kutokana na kitendo hicho, amechukua sampuli ya mafuta hayo na kuyapeleka Mombasa, Kenya kuyapima ili kugundua yana kiwango cha mafuta masafi kwa asilimia ngapi.
Alisema kuwa malori hayo yana uwezo wa kupakia lita 26,000 za mafuta lakini wahusika wanadai kuwa yanaweza kupakia lita 9,000 tu.
“Mafuta haya huibwa wakati yakitolewa katika meli na kupelekwa katika magari, karibu asilimia mbili nzima ya mafuta huibwa, kiwango ambacho ni kikubwa sana,” alisema.
Alisema kutokana na hali hiyo ameagiza kurejeshwa kwa kifaa cha kupimia wingi wa mafuta katika malori ya mafuta, ndani ya mwezi mmoja kuanzia jana.
Aanika ufisadi
Alisema kampuni ya Singirimo iliyopewa zabuni ya kusafirisha mafuta machafu, mkataba wake ulishaisha siku nyingi, lakini bado inaendelea na kazi hiyo na kwamba mwaka 2008, Ikulu iliwahi kueleza kuwa kampuni hiyo ni kinara kwa kusafirisha mafuta masafi na kudai machafu.
“Kampuni hii kila mwaka inashinda tenda ya kusafirisha mafuta tu, hivi sasa inachunguzwa na Ewura na Takukuru, nimeagiza mamlaka husika kwamba kampuni hii isijihusishe tena na usafirishaji wa mafuta ili kupisha uchunguzi,” alisema Dk Mwakyembe na kuongeza:
“Kampuni iliyokuwa namba mbili katika utoaji wa tenda ndiyo ipewe jukumu hilo na kama isipopewa ndiyo nitajua kuna kitu kinaendelea.”
Alisema kuwa mwaka 2008 Ikulu ilisema kuwa kampuni ya Singirimo ni ya wafanyakazi na vigogo wa TPA na inasafirisha mafuta masafi na kudai kuwa ni machafu.
Tuesday, July 31, 2012
Zitto ahojiwa kwa rushwa
SAKATA
la wabunge kuhusishwa na rushwa limeingia sura mpya, baada ya Naibu
Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Zitto Kabwe kuhojiwa na chama chake cha
Chadema kwa saa tatu jana.
Wakati Zitto akihojiwa, kambi rasmi ya upinzani bungeni, iliwataja wabunge saba wa CCM na kueleza kuwa ndiyo wanaolichafua Bunge kwa kujihusisha na mambo yenye maslahi binafsi wakiwa watumishi wa umma. Kadhalika, Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai alisema kwamba Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa (Takukuru) ilikuwa ikiendelea kuwahoji baadhi ya wabunge kuhusu tuhuma za rushwa na kwamba uchunguzi ukikamilika taarifa zitawekwa wazi. Zitto ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, jana aliandika katika ukurasa wake wa mtandao wa Tweeter kwamba alihojiwa na Sekretarieti ya chama chake kutokana na tuhuma za rushwa zinazowagusa badhi ya wabunge. Katika maelezo yake, Zitto alisema aliiambia sekretarieti ya chama hicho kwamba Chadema kifanye uchunguzi ili kubaini ukweli wa suala hilo na kwamba yuko tayari kuwajibika ikiwa itathibitika kwamba alihusika kula rushwa. “Kwa saa tatu nimejieleza mbele ya sekretariati ya chama kuhusu tuhuma za rushwa dhidi yangu. Niliomba kutaka kutoa maelezo kwa Katibu Mkuu, nimekiomba chama kufanya uchunguzi na ikibainika hatua zichukuliwe,” inasomeka sehemu ya taarifa hiyo kwenye Tweeter. Lissu ataja wengine Kwa upande wake, Mnadhimu Mkuu wa kambi hiyo, Tundu Lissu aliwataja wabunge wa CCM ambao wanatuhumiwa kuwa ni Nasir Abdallah (Korogwe Mjini), Mariam Kisangi (Viti Maalumu), Vicky Kamata (Viti Maalumu) na Charles Mwijage (Muleba Kaskazini) ambao hata hivyo, wote wamekanusha madai hayo. Wabunge wengine watatu tumeshindwa kuwataja kwa kuwa hawakupatikana kuzungumzia tuhuma dhidi yao. Katika orodha hiyo wamo wawili wa Viti Maalumu na mmoja wa jimbo na Lissu alidai kwamba wamekuwa wakishiriki vikao vya Kamati ya Nishati na Madini huku wakijua kuwa wana maslahi binafsi na wengine kutumia fursa hiyo kujinufaisha. “Kwa takriban juma moja sasa kumekuwa na mjadala mzito wa ufisadi hapa bungeni, sasa Kambi Rasmi ya Upinzani imejitathmini na kuona kwamba wabunge wake hasa walioko kwenye Kamati ya Nishati na Madini iliyovunjwa, John Mnyika, David Silinde na Mwanamrisho Abama hawahusiki,” alisema Lissu na kuendelea: “Ila uchunguzi wetu umefanikiwa kupata majina ya wabunge wanaohusika moja kwa moja na mgongano wa kimaslahi ambao tunaona tuwataje kwa maslahi ya umma.” Lissu alikwenda mbali zaidi na kutaja tuhuma zinazowahusu wabunge hao akisema wawili ambao gazeti hili halikuwaja, wamejihusisha kufanya biashara na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) hivyo wana mgongano wa kimaslahi. Alisema Mwijage ana mgongano wa kimaslahi katika mchakato mzima wa kuipa zabuni ya kusambaza mafuta kampuni ya Puma Energy kwa kuwa yeye ni mtalaamu mwelekezi wa kampuni hiyo inayomilikiwa na Serikali kwa asilimia 50. “Nasir Abdalah na Mariam Kisangi; Hawa wanamiliki vituo vya mafuta. Sasa kwa namna yeyote ile kuwa wajumbe wa Kamati ya Nishati na Madini hawawezi kutenda haki katika mchakato wowote unaohusu suala la mafuta,” alisema na kuendelea; "....(jina limehifadhiwa) hana mgongano wa moja kwa moja wa maslahi, lakini kwa kadri tunavyofahamu, yeye ndiye aliyekuwa akiyafanyia kampeni ya kupata zabuni makampuni ya mafuta ya Oryx na Camel na ....(jina limehifadhiwa), suala lake ni complicated kidogo. Maslahi aliyonayo katika suala hilo ni kuwa ana uhusiano wa Kimapenzi na kigogo mmoja katika Wizara ya Nishati na Madini.” “Hawa ndiyo wajumbe wa Kamati ya Nishati na Madini ambao sisi Kambi ya Upinzani tunawafahamu kuwa ndiyo waliojihusisha na mgongano wa kimaslahi. Tumewaangalia wabunge wetu wote watatu hawamo ila kama kuna mtu ana taarifa zinazowahusu, aseme na tutazifanyia kazi.” Lissu alisema kitendo cha wabunge kujihusisha na mgongano wa kimaslahi na taasisi za umma ni kinyume na Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma ya mwaka 1995 na ni kinyume na maadili ya kibunge. Katika hatua nyingine Lissu amemshauri Spika wa Bunge Anne Makinda kuzivunja pia kamati za Bunge za Serikali za Mitaa (LAAC) na Kamati ya Mashirika ya Umma (POAC) akisema nazo zina madudu mengi. “Hili lisiishie tu kwa kuvunja Kamati ya Nishati na Madini, tunataka pia kamati za POAC na LAAC zivunjwe, uchunguzi ufanyike na wahusika waitwe kujitetea na hatimaye wenye hatia watajwe hadharani bungeni na majina yao yachapishwe kwenye magazeti ili haki itendeke,” alisema. Alipoulizwa Chadema imefanya nini dhidi ya Mbunge wake, Zitto Kabwe kutajwa katika orodha hiyo, alijibu: “Nikiri kwamba sisi taarifa tunazo ila hatujamwita kumwuliza. Naomba ieleweke kwamba kama chama au Kambi Rasmi ya Upinzani hatuna maslahi na mbunge yeyote anayeonekana kujihusisha na masuala hayo.” “Katika hili tunaomba uchunguzi ufanyike na matokeo yake yatangazwe ili tupate msingi wa tuhuma hizo na ninaahidi kwamba tutazifanyia kazi ipasavyo.” Majibu ya tuhuma Alipotakiwa kuzungumzia tuhuma hizo, Kisangi alikiri kumiliki kituo cha mafuta lakini akasema sheria haimzuii mtu kama mambo yake anayafanya kwa uwazi. “Nimekuja bungeni nikitokea kwenye ualimu, nilikuwa nafundisha Shule ya Msingi ya Mianzini na biashara hii ni ya familia. Inaendeshwa kwa uwazi na mwanangu wa kwanza ndiye anayeisimamia. Kutokana na uwazi katika shughuli zangu, mwaka jana Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma ilinipongeza. Mimi ni msafi na siko huko wanakofikiri wao (Chadema).” Kwa upande wake, Mwijage alikanusha kuwa mtaalamu mwelekezi wa Kampuni ya Puma, badala yake akasema ni mtaalamu wa petroli anayefanya kazi ya kuishauri Serikali kuhusu mambo mbalimbali yanayohusu nishati hiyo. "Siyo kweli, hawa wanadandia hoja. Mimi ni mtaalamu wa petroli ambaye mchango wangu kimsingi una faida kubwa bungeni na hata kwa jamii kwa ujumla. Sijafanya maamuzi yeyote ya kulihujumu taifa hili na hata kwenye Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini pekee, nilitoa mchango wa kurasa 10 kuhusu masuala hayo ya petroli,” alisema Aliishauri kambi hiyo ya upinzani kuvuta subira, akieleza kuwa jambo lililoko bungeni linahusu ufisadi na uhujumu uchumi hivyo kauli zinazotolewa bila utafiti zinaweza kuvuruga mchakato mzima uliokwishaanzwa na Kamati ya Maadili ya Bunge. Awali, Abdallah alipoulizwa kuhusu tuhuma za kumiliki vituo vya mafuta hivyo kuwa na maslahi binafsi, alicheka na kuahidi kwamba angepiga simu baadaye, lakini hakufanya hivyo na alipopigiwa baadaye alikata simu. Hata hivyo, alizungumza na waandishi wa habari na kukanusha kumiliki vituo vya mafuta. Kamata kwa upande wake alisema: “Kuna kamati maalumu imepewa kazi ya kuchunguza mambo hayo, hivyo yote yanayoulizwa yatakuwa wazi na ukweli utajulikana tu. Nina maslahi au sina ukweli mtaujua, haraka ya nini?. Mjadala Bungeni Mjadala huo wa wabunge kuhusishwa na mgongano wa kimaslahi ulianza kulipuka bungeni jana asubuhi baada ya wabunge watatu; Joshua Nassari (Arumeru Mashariki), Salum Barwany (Lindi Mjini) na Mbunge wa Nkasi Kaskazni, Ali Kessy kutaka wabunge wanaotuhumiwa kwa ufisadi watajwe bungeni ili kuisafisha taasisi hiyo ya kutunga sheria. "Mheshimiwa Naibu Spika juma lililopita Mheshimwa (Vita) Kawawa alitoa hoja kutaka suala la ufisadi lishughulikiwe kwa kuvunjwa Kamati ya Madini na Spika akaridhia na kulipeleka suala hilo kwenye Kamati ya Maadili. Kwa nini Kamati nyingine zilizohusishwa na ufisadi huo nazo zisivunjwe?” alihoji Nassari na kuendelea: “Kuna Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) inayoongozwa na Mheshimiwa Mrema na Kamati ya Mashirika ya Umma (POAC) inayoongozwa na Zitto. Kuna tabia ya wabunge kuzikimbia kamati zisizokuwa na mikataba kama Kamati ya Huduma za Jamii na wanazikimbilia kamati zenye mikataba.” Barwany alitaka Bunge litajiwe majina ya wabunge waliotuhumiwa kwenye kashfa hiyo mpaka wakapelekwa kwenye Kamati ya Maadili, akieleza kuwa hili litasaidia kulisafisha... “Tumeambiwa Kamati ya Maadili inajadili suala hilo, lakini hatujatajiwa ni wabunge gani waliopelekwa huko, tunaomba mtutajie ili Bunge lijisafishe.” “Mimi naungana na wazo la Barwany na Nassari. Majina yatajwe wabunge tunadhalilishwa na wananchi huko mitaani. tuwataje hadharani,’ alisema Kessy. Akitoa mwongozo wa hoja hiyo, Ndugai aliiagiza Kamati ya Uongozi ya Bunge kutoka kwenye ukumbi wa Bunge ili wakajadili suala hilo na baadaye apelekewe taarifa. “Naamini wenyeviti wote wa kamati mmo humu ndani, naomba sasa hivi mwende kwenye Ukumbi wa Spika mkajadili suala hilo halafu nipate majibu sasa hivi,” alisema. Baadaye jioni, Ndugai alisema kuwa Spika hawezi kuwataja kwa majina wabunge ambao wanajihusisha na rushwa kwa kuwa hawajui. Alisema Kamati ya Uongozi iliyokutana jana mchana ilikubaliana kuwa ufanyike uchunguzi wa kina kwa ajili ya kuwabaini wale wanaoshukiwa na kwamba ikibainika Bunge litawaanika hadharani. “Kamati imerejea kumbukumbu za hansard ya Jumamosi kuwa ufanyike uchunguzi wa kina juu ya jambo hilo na wabunge mtaitwa kwa ajili ya kutoa ushirikiano, ikumbukwe kuwa mbunge akiitwa siyo kwamba ndiyo amekuwa mtuhumiwa, bali pale itakapothibitika majina yatawekwa hadharani,’’ alisema Ndugai. Naibu Spika alitahadharisha kuwa ndani ya Kamati hiyo utafanyika uchunguzi wa kutosha kubaini kama kuna mjumbe mwenye maslahi kwa wale wahusika basi ataondolewa ili kutoa nafasi kwa kamati kufanya kazi yake ipasavyo. Aliwatahadharisha wabunge kuwa Kamati hiyo haitaingilia utaratibu wa vyombo vya dola ambao wamekuwa wakiufanya ikiwemo wa Takukuru wa kuwahoji baadhi ya wabunge.
source gazeti la mwananchi
|
Sunday, July 29, 2012
SABRI mC HIP MICHANO.mp3
I'm listening to SABRI mC HIP MICHANO.mp3 in Hulkshare:click here
Get ready for a new Artist Sabri a.k.a Brino with a new track call Mc hip Michano
Get ready for a new Artist Sabri a.k.a Brino with a new track call Mc hip Michano
Friday, July 27, 2012
FFU watoa wito kwa watanzania kuwapa shavu wanamichezo wetu !Olympic
Watanzana wameombwa kujitokeza kwa wingi katika kuwashingilia wanamichezo watanzania wanaoshiriki
katika michezo ya Olympic huko London, wito huo umetolewa na bendi maarufu ya Ngoma Africa aka FFU,
yenye makao yake Ujerumani.
Bendi ya Ngoma Africa inawaombea mafanikio na ushindi wanamichezo wa
Tanzania,
Tuwaomba watanzana
na marafiki wa Tanzania pamoja taha sisi mbali mbali zilizopo Uingereza na ughaibuni
kujitokeza kwa wingi na kuzipeperusha bendera za Tanzania kwa kuwashingilia wanamichezo wetu,kwa shangwe,
shangwe na mayoe ! Tanzania ! Tanzania! Tanzania! oyeeeeeeeeeee!
Mungu wabariki wanamichezo wetu! www.ngoma-africa.com
Mungu Ibaraiki Tanzania !
FFU Kuvuna walichopanda Ughaibuni!
Ngoma Africa band kupewa Tuzo la kimataifa,
" IDA - International Diaspora Award"
Habari za uhakika zinatonya kuwa bendi maarufu ya muziki wa dansi
barani ulaya "The Ngoma Africa Band" au maarufu kwa jina la "FFU"
wazee wa virungu na makombora ya muziki,yenye makao yake
nchini Ujerumani, Bendi imetajwa kuwa ni bendi bora inayoitangaza miziki
ya
Afrika kwa kasi duniani,na imechaguliwa kupewa tuzo maalumu
la
" IDA - International Diaspora Award" award , hiyo inatolewa na
tahasisi za kimataifa,itakabidhiwa kwa kiongozi wa bendi hiyo Kamanda
Ras Makunja wa FFU mwanzoni mwa mwezi wa nane.
Inasemekana Sherehe za kukabidhiwa TUZO hiyo zitafanyika mjini Tubingen,
mkoa wa Baden württemberg, kusini mwa ujerumani.
Tahasisi za kimataifa zinazoshughulika na utamaduni wa kimataifa kuanzia
mwaka jana zilianza mkakati kutafuta bendi ya kiafrika
inayolitangaza bara
la Afrika kwa kutumia muziki, na kuweka utaratibu
wa kuzipigia kura bendi
hizo katika tovuti mbali mbali online na offline,Ngoma Africa Band ikajichulia
ushindi wa mamlioni ya kura, pia imegundulia kuwa bendi hiyi inakubalika na
mamilioni ya washabiki wa mataifa mbali mbali,
Mzimu huo wa muziki kutoka Bongo unadaiwa kuwa na wafuasi milioni
50 duniani kote,hali hii inatishia maporomota wa muziki wa kimataifa,
kuwa FFU ni mali ya mamilioni ya
washabiki,ni bendi ambayo kipenzi
cha mamilioni ya washabiki. katika kambi yao hii
www.ngoma-africa.com
inakadiliwa kuwa na mamilioni ya lank.
Tunawatakia kila yaliyo mema vichaa wetuSaturday, July 14, 2012
Monday, July 9, 2012
BET Awards 2012 Jay-Z, Beyoncé, Kanye West and Kim Kardashian.
After standing to congratulate Kanye on his win, Kim watched eagerly as Jay and 'Ye accepted the BET Award for Best Group.
During their speech, Yeezy thanked fellow rap labels Young Money and MMG for boosting his music-making ambitions and gave a special nod to rapper Big Sean for winning the award for Best New Artist.
Madea's Witness Protection.
Box Office: Ted, Magic Mike Edge Out Madea
Seth MacFarlane's comedy had best opening ever for R-rated film.
Family Guy creator Seth MacFarlane's first feature film venture Ted smashed records with a $54.1 million take and the No. 1 crown: the best performance in history for an R-rated comedy. The Mark Wahlberg starrer (his co-star is a human-like teddy bear) easily beat the other new entries this weekend, Magic Mike and Madea's Witness Protection.
But Mike had plently of dollar bills stuffed into its G-string, to the tune of $39.2 million and way better than expected (unless you ask anyone interested in seeing Channing Tatum's bare chest) for an R-rated film.
Coming in third place was Tyler Perry in Madea's Witness Protection. Though the film couldn't compete with talking bears and shirtless men, it did pull in an impressive $26.4 million.
On the indie film end of the spectrum, Sundance winner Beasts of the Southern Wild opened to strong numbers in four theaters in New York and Los Angeles, and is expected to roll out to other cities in the coming weeks.
Next week, The Amazing Spider-Man goes head-to-head with Oliver Stone's Savages for the most Fourth of July box office fireworks.
Morgan Freeman Says U.S. Still Has No Black Presiden
The Oscar winner says Barack Obama’s white “mama” only makes him mixed race.
While talking to NPR about his latest movie, The Magic of Belle Isle, the conversation turned to politics and the President's critics. That's when the actor said he thought Obama should not be called America’s first Black president.
“First thing that pops into my head regarding our president is that all of the people who are setting up this barrier…they just conveniently forget that Barack had a mama, and she was white — very white American, Kansas, middle of America,” Freeman told NPR. “There was no argument about who he is or what he is. America’s first Black president hasn’t arisen yet. He’s not America’s first Black president — he’s America’s mixed-race president.”
In the interview, The Dark Knight Rises star goes on to say that he has been disappointed by the Republican Party and Obama opponents' unfair treatment of the President. But Freeman's comments about the Obama's level of Blackness — which will certainly be viewed as offensive by many — opens a Pandora's box discussion on race. Like, when did being biracial not make you Black? Shouldn’t it be a biracial person’s choice to choose how he or she is identified? And can there ever be an all-“Black” president in this country given America’s race mixing history due to slavery?
Maybe one day Freeman will elaborate more fully on this topic. In the meantime, comments by website and blog commenters should definitely fill the void.
Usher step - son has declare brain dead
UPDATE: Kyle Glover, son of Tameka Foster and stepson of Usher, has been declared brain dead by doctors at an Atlanta children's hospital, TMZ reports. The 11-year-old was airlifted there after being hit by a jet ski in Lake Lanier, and has not experienced any brain activity since.
Usher arrived at the hospital late last night to join his estranged wife Tameka, who hasn't left the critical care unit since she arrived yesterday afternoon.
No decision has been made as to whether or not to take Kyle off of life support.
PREVIOUS: Kyle Glover, the 11-year-old son of Usher's estranged wife Tameka Foster, has been rushed to an Atlanta hospital following a jet ski accident today, TMZ reports. He's in currently in critical condition.
According to sources, Glover was struck by a jet ski while lounging in an inner tube on Lake Lanier and hit in the head. He was unresponsive when taken out of the water and remained that way when he reached the hospital.
TMZ reports that Usher chartered a plane for his ex, who was out of town, so she could rush to her son's bedside. Despite their ongoing divorce drama, sources say Tameka is extremely grateful to Usher for the gesture and is currently at the hospital anxiously awaiting further news about Glover's condition.
Prayers go out to Kyle Glover and his family for a quick recovery.
Monday, May 28, 2012
Mlevi alawitiwa mpaka kufa baa
kijana mmoja kwa jina analofamika kama Adam Mustapha mkazi wa Mbagala ambaye picha zake hapo alfajiri ya leo umekutwa amekufa katika baa moja kwa jina maarufu Dar live ndogo or Double K.
Kijana ambaye amekutwa akiwa na mizinga miwili ya kunyagi na pia mbegu za kuime ambazo mashaidi waliokuwepo katika eneo hilo wa nyumba za jirani walimsikia kijana huyo akipiga kelele wameiambia blog hii kwamba walimkuta akiwa amelawitiwa na kustili kwa kumfunika na kitenge hicho mpaka naondoka eneo la tukio polisi ndo walikuwa wamefika mida ya saa 2 asubuhi kuchukua mwili wa marehemu ,
Habari za kufahamika marehemu alikuwa mfanyakazi wa A.M STEEL ambacho ni kiwanda cha nondo
Sunday, April 29, 2012
Exclusive! Nas Talks About Performing With Jay-Z and Alicia Keys at Carnegie Hall
Alicia said that the recent show at Carnegie was a dream come true, in a big part because you have ALWAYS been one of her favorite artists of all time. She said it was a total New York moment to be somewhere so prestigious, and with you there. What was it like for you?
Nas: Carnegie Hall was incredible for a couple of reasons. I told Jay, look at us, two dudes from the projects on one of the most historic stages in the world. [We were] wearing tuxes, drinking vintage wine and champagne, on stage! That's how you do it. Alicia was amazing. The feeling I had being on stage with her and Jay is beyond words in the dictionary. I couldn't believe it. It was so Rat Pack. It's no joke to be the one who creates the official song for the greatest city in the world. Alicia helped make this timeless. "Empire State of Mind" song is a official New York anthem and Alicia keys helped to make it epic.
You've worked several times together over the years. She spoke to me a lot about how much she has changed, and how much her music has changed especially recently. What was Alicia like when you first met her? And what changes have you noticed?
I met Alicia before the world knew her. She was still on Columbia. Not on J Records with Clive yet… [the late '90s]. I don't know if she remembers this but, it was summer time in New York, me and my guys were looking for some place to go out to and we struck up a conversation with her and her girls. And after that I have just watched her do her thing. Now, after we thought all the slots in the music scene were taken... Alicia has showed us the missing key, the cute around the way girl meets, the edge of Tina Marie, and the soulful classiness of Ray Charles.
Do you think in the radio world now, where everything is so pop, there's room for her?
I would say it makes it even better for her because there is only pop. She is a REAL artist in a pop world. This gives her the opportunity to never need to fake it bc authenticity is what people search for in music. She has that.
Alicia is super funny in person. Any stories you can share about her that reflect her true personality?
She's creative. At Carnegie hall it was her idea to stay on stage for "Empire State of Mind" through "New York State of Mind." It made the performance and homage to NY that much more for the three of us to be up there.
Musician Recaptures Tanzanians Lost Glory
anzania has regained its lost glory in world of music fame that has dwindled since the eighties.
When the name of Tanzania is currently mentioned in international
music circles the name of Ebrahim Makunja popularly known as Ras Makunja
of FFU and his “The Ngoma Africa Band” aka FFU based in Germany cannot
be slighted. FFU has earnestly strived to place Tanzania in the
international music charts.
It is the only Tanzanian band that is based overseas. Its
contribution in the music industry both in Tanzania, East Africa and
abroad is superb. The band has often been able to bring its records to
radio stations back at home.
Many of their hits touch the souls of their fans. Two of their hits,
which are very popular in local radio stations and contained in “50
Uhuru Anniversary” CD are “Shangwe”, and “Miaka 50 ya Uhuru”. The rumba
style songs are composed by band leader Ras Makunja.
He pairs in singing with the comical solo guitarist Chris-B. Apart
from the well composed lyrics and the highly perfected musical beat the
songs carry very strong and emotional messages to the community. Their
messages are acclaimed not only in Tanzania but world all over.
Ras Makunja of FU, is not only a seasoned tactful and artistic
composed. He too has visionary messages to the society. To call him
Kamanda (Commander) Ras Makunja is not demeaning him.
He ensured that two of his CDs including “Jakaya Kikwete 2010″ which
claimed global fame reached more than 310 radio stations in the world.
This CD earned him the mark of being a hard headed musician from some
quarters.
His band now dubbed FFU (Fanya Fujo Uone) literally means creates
chaos and see, immediately came up with a CD “Anti Corruption Squad”
which has the song “Rushwa ni Adui wa Haki”. The fans see this song as
the Al-Albadir of the corrupt.
The song was a smash hit within Tanzanians. It placed Ras Makunja and
his band ‘Ngoma Afrika’ not only as ordinary musicians in the musical
arena. They had something else to offer the society apart from the usual
entertainment. Visionary eye opening and soul searching messages.
Yet despite all this no one seems to realize the onerous task that
this musicians does. They have never been ordained with a single medal
here at home. As a popular Swahili goes “Asiyekuwepo na lake halipo” (He
who is not there (present) so is his/her share). Ras Makunja and Ngoma
Afrika may not be with us, but his works and messages are!
The official web of the band is www.ngoma-africa.com One can become a
fan member of the band by signing up. The good work the band is doing
in promoting Tanzania in the field of music deserves local support both
in cash and form.
Wednesday, April 11, 2012
Elizabeth Michael (Lulu) aongea na polisi
MSANII Elizabeth Michael (Lulu), ameiambia polisi
kuwa kifo cha Steven Kanumba kimetokana na ugonvi kati yao, huku taarifa nyingine zikieleza kuwa huenda Lulu akafikishwa mahakamani leo. Habari zilizopatikana jana kutoka Kituo cha Polisi Oysterbay zilieleza kuwa, Lulu alisema kuwa kulitokea ugomvi kati yake na Kanumba baada yeye kuzungumza na simu kutoka kwa mtu maarufu anayetajwa kuwa mpenzi wake. "Lulu alisema kuwa ugomvi ulitokana na simu aliyopigiwa na mpenzi wake mwingine, ambaye ni mtu maarufu nchini, ndipo Kanumba akamfokea na ndiyo ugomvi ukaanzia hapo," chanzo hicho kimesema. Chanzo hicho kiliongeza kuwa baada ya Kanumba kuanguka, Lulu alitoka nje na kuondoka kwa gari lake hadi maeneo ya Coco Beach, lakini baadaye daktari wa Kanumba alimpigia simu akimtaka arudi ili wampeleke hospitali. "Alipororudi Sinza ndipo akakamatwa, lakini walikuja Kituo cha Polisi Oysterbay kuchukua PF3," kilisema chanzo hicho. Chanzo kiliongeza kuwa tangu Lulu alipofikishwa kituoni hapo amekuwa mtulivu asiye na wasiwasi wowote hata katika mahojiano na polisi. Katika hatua nyingine, Polisi wa kituo hicho jana walipata wakati mgumu baada ya kuibuka kundi la vijana waliotokea makaburi ya Kinondoni kumzika Kanumba, walioandamana wakidai wanamtaka Lulu. "Tunataka jembe letu", waliimba vijana hao waliofikia 100 wakitokea Barabara ya Ali Hassan Mwinyi huku wakishika majani na kufanya askari waliokuwapo kituoni hapo kuwahi kuchukua silaha na mabomu ya machozi kujiandaa kutuliza ghasia kama zingezuka. Hata hivyo vijana hao walitawanyika baada ya kuona askari wakiwa tayari kupambana nao na kukimbia maeneo mbalimbali. Katika hatua nyingine Patricia Kimelemeta anaripoti kuwa, Msanii Elizabeth Michael maarufu kwa jina la Lulu huenda akafikishwa mahakamani leo kujibu tuhuma za kuhusika na kifo cha Steven Kanumba. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela aliliambia gazeti hili jana kuwa Lulu atafikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni mara baada ya polisi kupata ripoti ya vipimo kutoka Mkemea mkuu wa Serikali. “Tunasubiri ripoti ya Mkemia Mkuu kubaini chanzo cha kifo hicho kwa sababu wamechukua baadhi ya sampuli za marehemu kwenda kupima na kwamba tutakabidhiwa leo(jana). Kimsingi tukipata tu taarifa hiyo tutamfikisha mahakamani,” alisema Kenyela. Aliongeza ripoti hiyo itaweza kuwasaidia kuandika mashtaka ili yaweze kufikishwa kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kwa ajili ya kumfikisha mahakamani. Kamanda Kenyela alisema kuwa, ripoti ya madaktari imewasilishwa juzi na kwamba imeonyesha kuwa Kanumba amefariki kwa ugonjwa wa mtikisiko wa ubongo.
Kauli mbili tofauti za Seth
Alipohojiwa na waandishi wa habari, Jumamosi asubuhi, Seth alisema Kanumba alifika nyumbani akiwa na Lulu saa sita usiku wa kuamkia siku hiyo wakiwa wanazozana wakaingia chumbani lakini hazikupita dakika tatu, Lulu akatoka na kumfuata Seth na kumwambia Kanumba amejipigiza ukutani amedondoka chini. Seth alisema alikwenda na kumkuta Kanumba akiwa chini huku povu likimtoka mdomoni akampigia daktari simu, ambapo baada ya kumpima, daktari huyo akashauri apelekwe Hospitali Muhimbili. Seth anasema wakati anakwenda hospitali alimwacha Lulu nyumbani na aliporudi hakumkuta na hajui alishikwa vipi na polisi. Akihojiwa na vyombo vya habari mchana huo wa Jumamosi, Seth anasema baada ya kula chakula cha jioni, Kanumba alimwambia ajiandae waende klabu. Seth anasema alimwambia Kanumba kuwa tayari amejiandaa, Kanumba akasema nisubiri. Kanumba akaingia chumbani, ghafla akasikia mlio wa gari, Lulu akashuka na kuingia ndani, akapitiliza moja kwa moja chumbani kwa Kanumba, baada ya muda mfupi, Seth akasikia mzozo chumbani, akaona kimya. Lulu akatoka akiomba msaada kwa Seth kuwa Kanumba kaanguka, aliingia akamkuta akiwa amelala chini hivyo akampigia simu daktari. Akasema wakiwa njiani wakapitia Kituo cha Polisi cha Oysterbay wakiwa na Lulu, baada ya maelezo, polisi wakamwambia Lulu abakie kwa ajili ya maelezo zaidi. Maswali ya kujiuliza 1. Kwa mujibu wa Kamanda Kenyela kifo hicho kilitokea saa 9 usiku, Je, Kanumba alimwambia mdogo wake wajiandae kwenda klabu muda huo? 2. Seth amezungumza kauli mbili tofauti za tukio hilo. Je, ipi ni taarifa sahihi? 3. Ni saa ngapi Seth na Kanumba walikuwa wanapata chakula cha jioni? 4. Kanumba alikuwa amerudi akitokea klabu au ndiyo alikuwa anataka kwenda klabu? 5. Hivi karibuni, Lulu alikaririwa na vyombo vya habari akisema hana mpenzi. Je, Kanumba alikuwa mpenzi wake? 6. Siku zote Kanumba alikuwa akidai hatumii kilevi chochote. Je, ni nani alikuwa anakunywa Jack Daniel's chumbani? 7. Je, Lulu alikimbia baada ya kifo cha Kanumba au aliambatana na Seth kwenda Muhimbili kabla ya Polisi kumshikilia katika kituo cha Oysterbay walipokwenda kufuata PF3? 8. Je, Lulu na Kanumba waliingia pamoja nyumbani kwa Kanumba au Lulu alikuja baadaye? 9. Lulu alikuwa anazungumza na nani kwenye simu na ni nini kilikuwa kinazungumzwa? 10. Lulu alikamatwa na polisi akiwa wapi? Msanii Stephen Kanumba alifariki usiku wa Ijumaa Kuu
Kwa habari zote kuhusiana na lulu na je? anakesi ya kujibu kuhusiana na kifo cha kanumba utazipata ndani ya blog hii
|
Saturday, April 7, 2012
Kanumba the great afariki..
Ni alfajiri kabisa kama saa 12 hivi watu wengine wakiwa ndio wanaamka na wengine wakienda kulala na kupata mshtuko wa kuondokewa na kipenzi chao kwenye tasnia ya filamu hapa bongo Steven Kanumba nyumbani kwake Sinza Vatcan ni kwamba kweli mwigizaji STEVEN KANUMBA amefariki dunia na inaaminika chanzo cha kifo chake ni baada ya kuanguka na kuanza kutoa mapovu hapohapo nyumbani kwake, alikua akiishi na mdogo wake anaitwa Fetty aliekua chumba kingine ambae amethibitisha kweli kwamba alimkuta kaka yake akiwa ameanguka.
Polisi wameondoka nyumbani kwa Kanumba muda mfupi uliopita baada ya kuwachukua waliokua wanaishi na Kanumba akiwemo mdogo wake Fetty ili kwenda kusaidia maelezo ya kilichotokea.
Bado watu wanazidi kuongezeka nyumbani kwa Kanumba ambapo tayari idadi kubwa ya wasanii wenzake wamefuka pamoja na watu mbalimbali,Ila kumekua na taarifa nyingine ambazo hazijathibitishwa kwamba Kanumba alianguka na kuumia kichwani baada ya mpenzi wake ambae anatajwa kuwa ni mwigizaji LULU kumsukuma na kuanguka wakati wanagombana.
‘Inasemekana’ Kanumba wakati akijiandaa kutoka saa sita usiku aliingia bafuni kuoga, alipotoka alimkuta Lulu akiongea na mwanaume mwingine kwenye simu ndipo alipokasirika na ugomvi kuanza.Kwa sasa msanii wa kike Lulu anashikiliwa na police kwa maelezo zaidi
Alipelekwa hospitali Muhimbili ambako muda mfupi baadae alifariki dunia, mwili wake bado uko katika chumba cha kuhifadhia maiti Muhimbili hospital
Labels:
herrylord3.blogspot.com
Location:
Dar es Salaam, Tanzania
Subscribe to:
Posts (Atom)