Kanumba the great afariki..
Ni
alfajiri kabisa kama saa 12 hivi watu wengine wakiwa ndio wanaamka na
wengine wakienda kulala na kupata mshtuko wa kuondokewa na kipenzi chao
kwenye tasnia ya filamu hapa bongo Steven Kanumba nyumbani kwake Sinza
Vatcan ni kwamba kweli mwigizaji STEVEN KANUMBA amefariki dunia na
inaaminika chanzo cha kifo chake ni baada ya kuanguka na kuanza kutoa mapovu
hapohapo nyumbani kwake, alikua akiishi na mdogo wake anaitwa Fetty aliekua
chumba kingine ambae amethibitisha kweli kwamba alimkuta kaka yake akiwa
ameanguka.
Polisi wameondoka nyumbani kwa Kanumba
muda mfupi uliopita baada ya kuwachukua waliokua wanaishi na Kanumba akiwemo
mdogo wake Fetty ili kwenda kusaidia maelezo ya kilichotokea.
Bado watu wanazidi kuongezeka nyumbani kwa
Kanumba ambapo tayari idadi kubwa ya wasanii wenzake wamefuka pamoja na watu
mbalimbali,Ila kumekua na taarifa nyingine ambazo
hazijathibitishwa kwamba Kanumba alianguka na kuumia kichwani baada ya mpenzi
wake ambae anatajwa kuwa ni mwigizaji LULU kumsukuma na kuanguka wakati
wanagombana.
‘Inasemekana’ Kanumba wakati akijiandaa
kutoka saa sita usiku aliingia bafuni kuoga, alipotoka alimkuta Lulu akiongea
na mwanaume mwingine kwenye simu ndipo alipokasirika na ugomvi kuanza.Kwa sasa msanii wa kike Lulu anashikiliwa na police kwa maelezo zaidi
Alipelekwa hospitali Muhimbili ambako muda mfupi baadae alifariki dunia,
mwili wake bado uko katika chumba cha kuhifadhia maiti Muhimbili hospital
No comments:
Post a Comment