Berlin,Ujerumani,
Umoja
wa Watanzania Ujerumani (UTU) unatarajia kufanya mkutano wake mkuu wa uchaguzi siku ya kilele cha sherehe za
muunganno wa Tanzania mjini Berlin, Ujerumani. siku ya tarehe 26.April.2014
kuanzia saa 7 mchana katika ukumbi wa Deutsche Bank, Unter den Linden 13-15, 10117
Berlin, Ujerumani.
Watanzania
wote wanaoishi Ujerumani wanaombwa kuhudhuria kwa wingi katika mkutano huu muhimu
wa chombo chao UTU ambao kinawaunganisha watanzania wote waishio ujerumani
bila kujali itikadi zao za kidini, jinsia, wala kabila.
Umoja
wa watanzania ujerumani unafuraha kubwa ya kuwafungilia milango wale wote ambao
wanataka kujiunga na umoja huo. Pia milango ipo wazi kwa wadau na wale wote
wanaohitaji ushauri juu ya kuwekeza au kuchangia maendeleo ya jamii nyumbani
Tanzania.
Pia pata kuwepo na vyakula vya kitanzania
KUFIKA
KWENU KATIKA MKUTANO HUU NDIO MAFANIKIO YA WATANZANIA WOTE
UMOJA
NI NGUVU , UTENGANO NI UDHAIFU
UMOJA
WA KITAIFA NDIO MSINGI IMARA KWA WATANZANIA
MUNGU
IBARIKI TANZANIA