Monday, October 29, 2012

brino-hip hop chapter [High quality].

 listening to brino-hip hop chapter [High quality].mp3 click here

Saturday, October 27, 2012

Watanzania wa Ujerumani Kukutana na wafadhili zaidi ya 150 ! huko Mainashaff,Ujerumani

UNION OF TANZANIANS IN GERMANY (UTU)
KUKUTANA NA WAFADHILI NA WAHISANI ZAIDI YA 150 !!!!
  WORLD MISSION SUNDAY 28.OCT. 2012
Umoja wa Watanzania Ujerumani (UTU)  Unapenda kuwakaribisha Watanzania wote wanaoishi ujerumani, Katika Hafla ya WORLD MISSION SUNDAY. itakayofanyika Katika ukumbi Uliopo Hauptstr. 30, D-63814 Mainaschaff Jirani sana na Mji wa Aschaffenburg Siku ya Jumapili Tarehe 28.10.2012, Kuanzia saa 04:00  za Asubuhi. Ambapo Wasamaria wema na Wafadhili wapatao zaidi ya 150 kutoka sehemu mbali mbali za ujerumani watakutana na umoja wa Watanzania Ujerumani (UTU) Juu ya kuitakia mema Tanzania na kuanzisha Harambee ya kuchangia maendeleo ya miradi mbali mbali itakayosimamiwa na Umoja wa watanzania Ujerumani (UTU). Katika Hafla hiyo Kuanzia saa  9 mchana watayarishaji wa Hafla hiyo ''World Mission Sunday'' itatoa nafasi kwa Umoja wa Watanzania Ujermani (UTU) Kuitambulisha Tanzania Kwa wahisani hao , na kuelezea ni mradi gani unahitaji  ufadhili kupitia Umoja huu.  Mmoja wa wageni rasmi walio alikuwa ni Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Mhe. Ahmada Ngemera, Dr. Lippert na mkewe Kutoka Scheinfurt' Dr. Lippert ni mtaalamu ambaye aliwahi kufanya kazi Tanzania. Hafla hii inategemewa kuisha saa 12:00 za jioni, baada ya hapo watanzania watapata muda wao wa kufanya mazungumzo na Mhe: Balozi wa Tanzania Nchini ujerumani Bw. Ahmada Ngemera.

Umoja wa Watanzania Ujerumani  UTU Umeramba Bingo kwa kupewa nafasi hii ya pekee  Na WORLD MISSION SUNDAY Kuiwakilisha Jamii ya watanzania na kuwashawishi Wafadhili na wahisani nchini ujerumani ili waweze kuchangia Miradi mbali mbali ya Huduma za jamii nchni Tanzania ikiwemo sekta ya Elimu na Afya.

Tunawaomba Watanzania Wote  na marafiki wa Tanzania  wanaoishi Ujerumani na jirani mwa ujerumani, kuhudhuria kwa wingi katika Hafla hii muhimu kwa jamii ya watanzani kama wasemavyo wahenga ''CHEREKO CHEREKO NA MWENYE MWANA'' Kwa maelezo zaidi wasiliana na
kamati.utu@googlemail.com au unaweza kuwasiliana na Mwenyekiti Wa UTU moja kwa moja kupitia simu ya mkononi. 0173-4298997
Karibuni sana ! Umoja Ni Nguvu
 
 

NURU FEAT VEDASTO - CHAPA LAPA

NURU FEAT VEDASTO - CHAPA LAPA

Monday, October 1, 2012

Dantiz Ft GQ - Near By ( Final-Official).

 listening to Dantiz Ft GQ - Near By ( Final-Official)... click here for download or listening
 Pata kumsikiliza dantiz walii na kitu chake kimya kabisa near by u kutoka Racers ngoma imeenda mbele sana

Umoja wa watanzania Ujerumani wapata Uongozi Mpya

Naibu Balozi Mh.Ali Siwa (mwenye suti nyeusi) akiwa na viongozi wa UTU.

watanzaia Ujerumani wakiwa na furaha ya umoja wao

Kamanda Ras makunja katikati,akipigwa pini na Sudu Mnete wa Radio DW (mwenye nyeusi na nyeupe) Mdau Elezius naye pembeni

Meza kuu katika mkutano wa Umoja wa watanzania Ujerumani.


Mhe.Bw.Ali Siwa (mwenye suti nyeusi) akiwa na viongozi wa UTU

Mwanadiplomasia Naibu balozi Bw.Ali Siwa (katikati)akiongea na watanzania.


Watanzania Ujerumani wakiduarika

huyu bint mdogo naye alikuapo

Sudu Mnete wa Radio DW (mwenye nyeusi na nyeupe)akiwa na viongozi wa UTU

Mkutano mkuu wa watanzania waishio ujerumani  uliofanyika siku ya jumaamosi tarehe 29. 09 2012 Mjini Frankfurt katika kitongoji cha Raunheim. ulifanikiwa kutimiza malengo yake na maazimio yake  Moja wapo ilikuwa ni kufanya uchaguzi wa uongozi wa umoja huo, kabla ya kufanyika uchaguzi huo na mjadala  wa maazimio ya umoja huo, Mgeni rasmi katika mkutano huo mwana diplomasia naibu balozi wa Tanzania nchini ujerumani mheshimiwa Bw. Ali Siwa alitoa nasaha zake na salamu kutoka Ubalozi wa Tanzania Nchini ujerumani kwa watanzania waliohudhuria katika mkutano huo, kwanza aliwapongeza watanzania kwa kufanikiwa kuunda umoja huo wa watanzania waishio ujerumani ambao ndio mwamvuli mkuu wa mshikamano wa watanzania wote nchini ujeruman, isitoshe Bw. Ali  Siwa aliwaambia watanzania kwamba ofisi yake ipo wazi wakati wowote iwapo umoja huo utahitaji ushauri wowote utakaoleta  maendeleo ya umoja huo na watanzania kwa ujumla, aliwaasa watanzania kuwa mshikamano wao na umoja wao ndio utakaokuwa ufunguo  na sauti ya maendeleo yao na vizazi vwao ugenini na nyumbani pia. baada ya nasaha hizo  wananchama wa umoja wa watanzania  walichagua viongozi wao kama ifuatavyo:-

Mwenyekiti: Mfundo Peter Mfundo, Makamo: M/Mwenyekiti. George Mtalemwa. Katibu: Bi Tulalumba Mloge. Muweka hazina: Bi Mwamvua Dugala Merkel.

Umoja huo wa Watanzania Ujerumani (UTU) ndio chombo pekee kilichopata usajili kwenye serikali ya ujerumani, na kutambuliwa kisheria,  ambacho kinawaunganisha watanzania wote wanaoishi ujerumani, na ndio Daraja linalowaunganisha  watanzania waliopo Nyumbani na kwengineko ughaibuni. Kwa watanzania wanaopenda kujiunga na umoja wa watanzania ujerumani (UTU) milango ipo wazi,  wasiliana na  kamati.utu@googlemail.com