Monday, October 3, 2011

CCM YASHINDA IGUNGA




Jumla ya kata katika jimbo la Igunga lenye wakazi 325,000 na wapiga kura 171,265 lina kata 26. Uchaguzi huo, unafanyika kuziba nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo, Rostam Aziz, aliyejiuzulu Julai 13 mwaka huu.Rostam alikuwa mbunge wa jimbo hilo kwa miaka 15 mfululizo kuanzia mwaka 1994.

Wagombea wanaowania nafasi hiyo ni Dk.Peter Kafumu wa CCM, Leonard Mahoma wa CUF na Kashindye wa Chadema. Wagombea wengine wanaoshiriki uchaguzi huo na vyama vyao kwenye mabano ni Said Cheni (DP), Hemed Dedu (UPDP), Hassan Rutegama (Chausta), John Maguma (Sau) na Steven Making.

Wagombea wote mbali na kujinadi kwa sera za kuwaletea maendeleo wananchi na jimbo hilo tangu kampeni hizo zilipoanza Septemba 7, mwaka huu

Matokeo ya Uchaguzi mdogo Igunga kata kwa kata

(Jumla kuu ni CCM 26266. CHADEMA 22443)

Mboto CCM 730- CHADEMA 302
Nguvu moja CCM 694 CHADEMA 284

Nkinga CCM1479. CHADEMA 1085

Itumba CCM1079 CHADEMA 590

Nanga. CCM 897. CHADEMA 645

Igurubi CCM 925 CHADEMA 592

Mwisi CCM 926. CHADEMA 992

Mbutu. CCM 1186. CHADEMA 1426

Kinungu. CCM 505 CHADEMA 268

Ngulu CCM 622 CHADEMA 412

Igunga CCM 3181 CHADEMA 3358

Choma CCM 1227 CHADEMA 918

Kining. CCM 700 CHADEMA 451

Mwashiku. CCM 798 CHADEMA 484
Nsimbo CCM 738 CHADEMA 1016
Itunduru CCM 738 CHADEMA 784
Mwamashimba CCM 1224 CHADEMA 1421
Mbutu CCM 1335 CHADEMA 1427

Bukoko CCM 1136 Chadema 931

Nyandekwa CCM 691 Chadema 631
Ndembezi CCM 866 Chadema 806
Chabutwa CCM 545 Chadema 581

Ziba CCM 1053 Chadema 860
I
goweko CCM 1051 Chadema 880

Sungwizi CCM 1225 Chadema 718

Isakamaliwa CCM 525 Chadema 593

Chama cha Mapinduzi CCM kimeibuka kidedea katika uchaguzi mdogo wa Ubunge jimbo la Igunga mkoani Tabora, Mgombea wa kiti hicho Dk Dalaly Kafumu ameongoza kwa kura 26,266 akifuatiwa kwa ukaribu na mgombea wa Chadema Joseph Kashindye mwenye kura 22,443 huku mgombea wa CUF Leopold Mahona akishika nafasi ya Tatu kwa kura 2000 tu.

Matokeo haya yemesomwa hadharani na msimamizi wa uchaguzi jimboni humo muda huu wa mchana. Awali Jimbo hilo lilikuwa chini ya Mbunge Rostam Azizi aliyeamua kujiuzuru.

No comments:

Post a Comment