Monday, June 27, 2011

RAHA NA KARAHA YA DALADALA



Bila daladala hujaizungumzia Dar es salaam zinakula vichwa vya maana, utamsikia konda akisema ''gari haijai, inajaa ndoo ya maji oyaa,ingia na viatu humo , siti za kulala '' wakati anasema hivyo basi limefurika hadi mlangoni na baada ya hapo linakimbia kwa kasi ya kufa mtu.Ni usafiri wa kila mtu wakubwa, kwa wadogo,wake kwa waume. Maeneo mengine utasikia mtu anasema ''nina miaka mitano sijawahi kupata siti'' usishangae ni kweli kuna mida ya hatari basi haijasimama ishajaa, usiulize wamepitia wapi, jibu ni dirishani ! lakini pamoja na yote hayo tunaenjoy usafiri wetu

No comments:

Post a Comment