Saturday, January 14, 2012

MBUNGE VITI MAALUM AFARIKI



Mbunge wa viti maalum mkoa wa morogoro kupitia tiketi ya(CHADEMA) Mh Rejia Mtema amepata ajali mbaya sana leo asubuhi katika eneo la Ruvu na kufariki dunia papo hapo wakati akiwa safarini kuelekea morogoro.

Mashuhuda walioshuudia ajali hiyo walisema kuwa mbunge huyo alikuwa anaendesha gari lake mwenyewe alipinduka na gari hio baada ya kumshinda wakati akijaribu kulipita gari linguine lilokuwa mbele yake katika eneo la Ruvu.

Ndani ya gari hilo kulikuwa na watu wengine wane ambao wamefikishwa katika hospitali ta tumbi kibaha.

Marehemu alikuwa waziri kivuri wa kazi na ajira na pia mbunge viti maalum kutoka kilombero mkoani mrorogoro

Mungu alaze roho ya marehemu mahara pema peponi amin


No comments:

Post a Comment