Saturday, July 30, 2011

KWELI NCHI IMEUZWA?



Ni kweli nchi imeuzwa au ni macho yangu na mawazo yangu tu ki ukweli ni miaka 50 sasa tumetimiza na tarehe 9 december mwaka huu ni kilele cha miaka 50 tangu uhuru wa nchii tangu tukabidhiwe uhuru kutoka kwa uingereza...Siku zote imani mbaya ya wanachi kwa serikali yao inaonyeshwa katika mazingira mabovu ya uchumi,mazingira pamoja na miundombinu mibovu lakini bado fikra zangu zinanishawishikusema kweli nchii hii imeuzwa kama kiwanja cha mpira wa kikapu anapewa muwekezaji ili aweke barabara kwamkataba wa miaka 100 sasa nchi tutakuwa tunaipeleka wapi kama tunaingia mikataba ya miaka mia mia inamaanisha taifa la sasa na la baadaye tunalipereka wapi ikiwemo vizazi vyetu vinavyokuja ki ukweli kama mwenye kesi ya rada mpaka leo yupo uraiani na sasa hawa wanaoingia mikataba mibovu kama RICHMOND,DOWANS.IPTL.KIWILA.TRL na mengine mingi wapo bado uraiani sasa nchi tunaipeleka wapi?
Ikiwa serikali imeshindwa kuwekeza kabisa katika miundombinu ya umeme na barabara katika miaka yote hii 50 wanatakakutuambia wanachi kwmba hakuna hata kiongozi mmoja aliyefikilia mbele na kusema siku moja ongezeko la watu litazidi nchiii hii nakumbuka katika awamu ya pili ya rais wetu mstaafu Benjamini wiliam mkapa alikuja na sera moja ya ubinafsishaji wa mashirika ya umma na kuwapa wawekezaji katika kuyaendeleza ili kwa wanavyodai masharika hayo yalikuwa yanaendeshwa kwa hasara,ki ukweli sikuwa najua uhali wa kauli ile lakini yote hayo katika ubinafsishaji kulikuwa na ungezeka la wawekezaji kutoka nchi mbalimbali duniani ambao walivutiwa na sera zetu

No comments:

Post a Comment