Saturday, July 2, 2011

MIM,TANZANIA NA UMEME



Tanzania ni nchi ambayo inaasilimali nyingi sana na nchi yenye kuvutia kwa kila mgeni anayetua hapa ila serikali yetu ya sasa na zilizopita walishindwa kujua nini umuhimu katika kuwekeza katika sekta nzima ya umeme au hata kubolesha ile miundombinu ya umeme iliyokuwepo tangu enzi za mkoloni.Nalia na swala zima la umeme linalotukumba nchi hii yenye utajiri mkubwa dhahabu,almasi,tanzanite,makaa ya mawe ulleniam pamoja na vivutio vizuri kama mbuga za wanyama,misitu ya asili pamoja na mlima kilimanjaro .
Najiuliza sana ni miaka 50 leo tangu tupate uhuru kutoka kwa uingereza hila katika miaka hiyo 50 tumeshindwa kabisa kusoma alama za nyakati katika swala la kuwekeza katika sekta hii nyeti kabisa katika maendeleo ya taifa letu hili...sipendi kuchukua nafasi hii kuilaumu tanesco ila naona hili ni kama janga la taifa zima na kunauwajibikaji mkubwa sana wa serikali kuliko hata tanesco yenyewe kama leo hii mgao unakuwa wa nchi nzima kwa masaa 10 na zaidi unawaweka wapi wale walioviwandani wakitegemea sana malipo ya siku(per day payment)wakiwa kama vibarua ni familia ngapi zitakuwa zimelala na njaa kwa tatizo la umeme ambao hauna muda maalum kukatwa wala kurudishwa,imekuwa kama desturi sasa umeme ukikatika hakuna anayeshangaa ila ukirudi ndo wanashangaa au kuwepo kwa umeme kuna kuwa kama ngushiro porini.najuuliza mimi,tanzania na umeme kuna nini kimejifisha najaribu kumtafuta mchawi ni nani yule aliyeingia mikataba mibovu ya umeme au Uzembe ya wale wachache ambao wameshika msumeno wa nchi hii.

No comments:

Post a Comment